Vitamin C Tablet
Viungo:
Vitamin C
Kazi Na Faida Zake
- Kuongeza kinga za mwili, kuongeza ukinzani wa mwili dhidi ya virusi, kuzuia mafua;
- Ni antioxidant yenye nguvu;
- Kulinda mfumo wa moyo na mishipa ya moyo;
- Kulinda na kupunguza kudhoofika kwa seli za macho (macula lutea), kunakosababisha ugonjwa wa kutoona vitu vizuri au upofu (macular degeneration) na mtoto wa jicho (cataract).
Yafaa Kwa:
Maelezo Muhimu:
Vitamini C, ambayo inajulikana pia kama ascorbic acid, ni vitamini muhimu kwa mwili wa binadamau. Inapatikana kutokana na matunda na mboga. Mwili wa binadamu hauwezi kutengeneza vitamini C, kwa hiyo lazima ipatikane kutokana na chakula. Hapa chini ni faida za kiafya za vitamini C. Mtu mzima mwenye afya anahitaji miligramu 75-90 za vitamini C kwa siku. Watu wanaovuta sigara wanahitaji miligramu 35 zaidi za vitamini kwa siku.
Kinga Za Mwili:
Kutumia vitamini C kwa wingi kunaweza kuimarisha leucocytes muhimu na kuongeza kinga dhidi ya vijidudu vamizi. Ni ya muhimu zaidi kwa ajili ya collagen, aina ya protini inayoapatikana katika mifupa, gegedu na tendoni. Matumizi ya vitamini C kwa kiwango sahihi yatailinda miili yetu dhidi vijidudu vamizi na kuifanya mifupa yetu na meno kuwa imara, na kuongeza kasi ya miili yetu ya kuponya vidonda.
Mafua:
Pamoja na faida za kinga za mwili za kupambana na bakteria, virusi, na maambukizi, vitamini C hufanya kazi kama antihistamine ambayo itazuia madhara ya mafua, uvimbe, kuzipa pua na maumivu ya kichwa.
Antioxidant
Vitamini C ni antioxidant yenye nguvu ambayo huzuia madhara ya radikali huru kwenye miili yetu. Madhara ya oksijeni kwenye miili yetu ni pamoja na atherosclerosis ambayo huleta magonjwa ya moyo na kiharusi, aina mbalimbali za saratani, pamoja na saratani za mapafu, midomo, koo, utumbo mpana, tumbo na umio.
Kinga Za Mwili:
.
itamini C husaidia katika utengenezaji wa vitamini E. br>
Magonjwa Ya Moyo Na Mishipa Ya Moyo:
Pamoja na kupunguza pressure, Vitamini C huhakikisha unyumbukaji wa mishipa ya damu, na kuzuia ujenzi wa tabaka za cholesterol kwenye kuta za mishipa ya damu, kwa hivyo kuondoa magonjwa ya moyo na mishipa ya moyo kama atherosclerosis, uzidifu wa cholesterol, moyo kushindwa kufanya kazi, na angina pectoris.
Kutoona vizuri Na Mtoto Wa Jicho:
Lensi ya jicho inahitaji vitamini C ili kufanya kazi vizuri, na ukosefu unaweza kusababisha mtoto wa jicho. Matumizi ya vitamini C kwa wingi yameonyesha kuzuia mtoto wa jicho kwa kupeleka damu kwa wingi kwenye jicho. Utafiti umeonyesha kuwa vitamini ikiambatana na virutubishi vingine inaweza kusaidia tatizo la kudhoofu kwa seli za mcho (age-related macular degeneration AMD) linaloanza kutoingia kwenye hatua mbaya zaidi.
<<<<< MWANZO